post-feature-image
HomeBurudani

WANAFUNZI WATUPWA JELA MIAKA SITA KWA MAUAJI YA MWALIMU WAO

Vijana wawili waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chemchem wilayani Mkalama katika Mkoa wa Singida, wamehukumiwa kifungo cha ...

Wastara kuwa mpenzi wa JB ndani ya filamu mpya ‘Mzee wa Swaga’ - Picha
Wasanii wa Kigoma wairudia ‘Nakula Ujana’ ya Nay katika mahadhi ya gospel - Nasali Sana
Dogo D amdiss Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, Mo asema kuna watu wanampotosha - Audio
Vijana wawili waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chemchem wilayani Mkalama katika Mkoa wa Singida, wamehukumiwa kifungo cha miaka sita kila mmoja baada ya Mahakama kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya mwalimu wao.
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma inayoendesha vikao vyake mjini Singida, ilitoa hukumu hiyo jana.
Waliohukumiwa ni Shani Mtua na Mohammed Salimu ambao  wakati walipotenda kosa hilo, mwaka 2008,  walikuwa Kidato cha Tatu na walikuwa na umri wa miaka 18 kila mmoja.
Ilielezwa mahakamani kwamba kulikuwa na washitakiwa wengine wawili katika kesi hiyo; Emmanuel Daud na Michael Msengi, walikufa wakiwa mahabusu  wakisubiri kesi yao kusikilizwa na Mahakama Kuu.
Hukumu  ilitolewa na Jaji Rehema Mkuye baada ya washitakiwa hao kukiri shitaka la kuua bila kukusudia walilofanya katika Kijiji cha Mpambala,  Tarafa ya Kirumi Wilaya ya Mkalama.
Awali, Mwanasheria wa Serikali,  Zakaria Elisaria aliyekuwa anasaidiwa na Karen Mrango, alidai mahakamani kwamba washitakiwa walihusika na mauaji ya  Rajabu Idude (49), aliyekuwa Mwalimu wa Nidhamu shuleni hapo. Ilidaiwa walifanya mauaji hayo  Agosti 2008.
Mwanasheria huyo wa Serikali alidai chanzo cha mauaji hayo ni mshitakiwa wa kwanza , Shani, kupewa barua ya kusimamishwa masomo kwa wiki mbili kutokana na utovu wa nidhamu na kisha akashawishi wenzake watatu kumpiga mwalimu huyo.
Zakaria alisema wanafunzi hao walimvizia mwalimu huyo katika kichaka cha karibu na shule yao wakampiga ngumi na mateke, kisha wakamjeruhi mwilini kwa kisu alichokuwa nacho mshitakiwa wa kwanza.
Inadaiwa kutokana na kipigo hicho,  Mwalimu Idude alipiga kelele na mwanawe aliyetajwa kwa jina la Maye Rajabu,  alifika haraka kwenye eneo la tukio, lakini akakuta ameshakufa.
Wanafunzi hao (washitakiwa) hawakukutwa katika eneo hilo lakini msako ulifanyika usiku huo na wanafunzi wanne walikamatwa. Baada ya kuhojiwa kuanzia ngazi ya mlinzi wa amani kwenye kijiji hicho hadi jana mahakamani, walikiri kosa.
Kwa upande wake, Wakili wa washitakiwa, kutoka Kampuni ya Uwakili ya  Kim & Company, Raymond Kimu, alimwomba Jaji Mkuye kutoa adhabu nafuu dhidi ya wateja wake, kutokana na kuonesha ushirikiano  wa kutosha tangu siku waliyokamatwa.
Aidha, alidai washitakiwa walifanya kosa hilo kutokana na kusukumwa na umri mdogo wa utoto. Alidai  ni wakosaji wa mara ya kwanza, wanajutia kosa hilo na kwamba wamekaa jela kwa muda mrefu wa miaka sita, hivyo wamejifunza kutokana na mauaji hayo.
Akitoa hukumu, Jaji Mkuye alisema hakuna ubishi kwa yote aliyosema wakili wa utetezi. Hata hivyo alisema, anadhani sababu hizo siyo kibali kwa washitakiwa hao kupanga na kutekeleza mauaji dhidi ya mwalimu wao aliyekuwa anasimamia nidhamu.
“Nadhani kosa walilofanya haliwezi kukubalika kwa  jamii hata kidogo…fujo zimekuwa zikitokea kwenye mashule na vyuo, hata kusababisha vurugu kiasi cha kuathiri utendaji…, kufuatia kosa hili, kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka sita jela,” alisema Jaji Mkuye.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: WANAFUNZI WATUPWA JELA MIAKA SITA KWA MAUAJI YA MWALIMU WAO
WANAFUNZI WATUPWA JELA MIAKA SITA KWA MAUAJI YA MWALIMU WAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCT2MhjxT1jaojAZSy9i81i3wqfUQVTfJNsV3vCnh7CUQrmE0PnN3HBX2SMllRrjvjPh_v0NiIaM3qYDixe1EsglIRWUG0Gx8feRrENZA4NfSs3iYHlzGUkgRGFam9RUC6-eF8wVaEYRM/s1600/jela.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCT2MhjxT1jaojAZSy9i81i3wqfUQVTfJNsV3vCnh7CUQrmE0PnN3HBX2SMllRrjvjPh_v0NiIaM3qYDixe1EsglIRWUG0Gx8feRrENZA4NfSs3iYHlzGUkgRGFam9RUC6-eF8wVaEYRM/s72-c/jela.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/07/wanafunzi-watupwa-jela-miaka-sita-kwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/07/wanafunzi-watupwa-jela-miaka-sita-kwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago