Rapper wa Mwanza mwenye umri mdogo aitwaye Dogo D amemdiss hitmaker wa ‘Basi Nenda’ Mo Music, Young Killer na N...
Rapper wa Mwanza mwenye umri mdogo aitwaye Dogo D amemdiss
hitmaker wa ‘Basi Nenda’ Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, kwenye
ngoma yake, Wamenichokoza.
Kisa cha kumchana Mo Music ni kutokana na kudai alitaka amshirikishe
kwenye wimbo wake aliourekodi kwenye studio za Classic Sounds zilizo
chini ya producer Mona Gangster lakini hadi leo amekuwa akimchenga.
“Mwanzoni ulipokwenda, pamoja tulikwenda, kuhit Basi Nenda kufanya
ngoma yangu ndio unanipiga kalenda,” anarap Dogo D kwenye wimbo huo
ambao ni muendelezo wa wimbo wa Nay wa Mitego, Wamenichokoza. Akiongea
kwenye kipengele cha Inbox kwenye kipindi cha Next Chapter cha Radio
Free Africa, Dogo amedai kuwa kila akimpigia simu Mo Music aende kuweka
kipande chake kwenye wimbo huo amekuwa akimpiga kalenda kwa sababu za
kuwa kwenye shows.
Kwa upande wake Mo Music amedai kuwa hajakataa kufanya chorus ya
wimbo huo bali ratiba zao zimekuwa zikichengana. Mo anasema yeye na
producer wake aitwaye Lollipop wamekuwa na mpango wa kumsaidia rapper
huyo kwa kugharamia miradi yake ikiwemo video na hivyo anashangaa
kumsikia Dogo akimdiss tena.
“Imani yangu sio yeye ndio maana siwezi kumchukia Dogo. Nahisi
alichokiandika it’s not Dogo D, yaani nyuma yake kuna watu wanampotosha,
hayupo hivyo namfahamu,” Mo Music ameimbia Inbox. “Kwahiyo wakamjaza
sumu kwasababu namfahamu Dogo D, ana love na mimi mpaka inapitiliza,
kwahiyo kuna watu wanamtengeneza.”
Sikiliza kipengele hicho hapo chini pamoja na kipande cha wimbo wa Dogo D.