Archive Pages Design$type=blogging

DIDA NDOA TENA! AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE

  Stori: Waandishi wetu SIKU chache baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani ku...


 
Stori: Waandishi wetu SIKU chache baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, ameonesha matumaini mapya ya kuolewa baada ya kumwanika mchumba’ke mpya.
 
Mtangazaji wa Kipindi wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida' akimlisha keki Shemeji yake, Feisal.
Dalili za matumaini hayo mapya zilionekana usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita katika sherehe yake ya kuzaliwa (bethidei) iliyofanyaka nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao Bongo. 
Khadija Shaibu ‘Dida' akiwa na mashemeji zake kutoka Arusha.
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria hafla hiyo ya
kufuru ni pamoja na malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa na waigizaji; Chuchu Hans, Jacob Steven ‘JB’, Rose Ndauka, Salma Salmin ‘Sandra’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Maimatha Jese na wengine kibao ambao walimpa Dida kampani ya nguvu na kumtunza fedha na zawadi mbalimbali. 
Shemeji, Feisal (mwenye kipaza sauti)  akiwasilisha ujumbe alioagizwa na mume mtarajiwa kwa 'Dida'.
Kama hiyo haitoshi, kwenye hafla hiyo, kulitawaliwa na vinywaji vya kila aina huku kukiwa akichinja mbuzi watatu maalum kwa ajili ya sherehe hiyo sambamba na kuku kibao wa kienyeji, nyama za kila aina, msosi wa nguvu na pombe za kumwaga. 
Miongoni mwa wageni waalikwa walikuwepo wasanii wa Filamu Bongo 'Chuchu Hans' na 'JB' .
Wakati sherehe ikiendelea, Dida aliibua minong’ono ya aina yake baada ya kutambulisha uwepo wa shemeji zake waliotoka Arusha ambao walimwakilisha mchumba wake katika pati hiyo.
“Jamani humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha, wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida. 
'Dida' akilonga machache kwenye Shrehe hiyo ya bethidei yake.
Ulipofika muda wa kutoa zawadi, mmoja wa mashemeji zake hao aliyejitambulisha kwa jina la Feisal alishika kipaza sauti na kusema alitinga kwenye hafla hiyo kumwakilisha ndugu yake (jina alilihifadhi) ambaye alimtuma amwambie Dida kuwa amemzawadia gari lenye thamani ya Sh. milioni 26 za madafu ambalo siku si nyingi litatua Dar.
“Hehee my new baby, huyo ndiye my new baby jamani na hawa ndiyo mashemeji zangu wa ukweli,” alipaza sauti Dida.
 
Ezden Jumanne wakati akiwa na 'Dida.'
Alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya mipango yake na mchumba huyo mpya, Dida alifunguka:
“Huyo ndiye mwanaume wangu wa sasa muda ukiwadia nitaanika kila kitu, bado mapema mno kuzungumza mengi,” alisema Dida ambaye kama ataolewa na mwanaume huyo itakuwa ndoa ya nne.
Dida aliyemwagana na Ezden Jumanne miezi kadhaa iliyopita, kabla ya hapo aliwahi kuolewa na wanaume wawili tofauti ambao alimwagana nao kwa talaka.
Waandishi: Mayasa Mariwata, Musa Mateja na Imelda Mtema/GPL

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: DIDA NDOA TENA! AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE
DIDA NDOA TENA! AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh67VPMSq1JR06Qy5j6H4d9MQvLxd0LzjiMOQKuksherOr5odcPIRzDMFgt0Jvr1Hme8GbSCfvMM0oJLF8gM6N3diinFYOjceIDNIID7-PmsWKvnukFe13B4OpUW05rNONe1KLNcnIGHVI/s1600/11.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh67VPMSq1JR06Qy5j6H4d9MQvLxd0LzjiMOQKuksherOr5odcPIRzDMFgt0Jvr1Hme8GbSCfvMM0oJLF8gM6N3diinFYOjceIDNIID7-PmsWKvnukFe13B4OpUW05rNONe1KLNcnIGHVI/s72-c/11.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/dida-ndoa-tena-amtambulisha-mchumba-wake.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/dida-ndoa-tena-amtambulisha-mchumba-wake.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago