Zuwena Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe Nuh Mziwanda wakipozi. IMEGUNDULIKA kuwa uhusiano wa staa wa Mduara, Zuwena Mo...
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe Nuh Mziwanda wakipozi.
IMEGUNDULIKA kuwa uhusiano wa staa wa Mduara, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’, na mpenziwe Nuh Mziwanda ni kazi bure kwani
uwezekano wa kufunga ndoa kati yao haupo kutokana na kupishana
imani.Ishu hiyo imejidhihirisha juzikati nyumbani kwa wawili hao
Mwananyamala-Manjunju jijini Dar, baada ya paparazi wetu kuwaibukia na
kutaka kujua malengo yao zaidi kama wana mpango wa kuoana au la, msikie
kwanza Nuh:
Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, akiwa na mpenziwe Nuh Mziwanda.
“Mimi ninampenda Shilole kwa asilimia 100, ila siko tayari kubadili
dini kwa ajili yake maana kwetu ni wakristo na hapa naongea mama yangu
ni mzee wa kanisa hivyo Shilole naamini anaweza kubadili maana mimi
tayari nimeshafanya mengi sana juu yake.”
Msikie Shilole: Mimi siwezi kubadili dini maana Nuh ndiye alisema
atabadili hata hivyo familia yangu haiwezi kunikubalia kubadili dini kwa
ajili ya kufunga ndoa kama amesema naye hawezi kubadili basi tutaishi
tu maana hata ndoa ya serikali yenyewe hawezi na maisha siyo lazima
tuoane.”