Diamond Platnumz ni msanii ambaye yuko kwenye level za juu kwenye kila kitu kwa sasa, upande wa muziki na hata aina ya maisha anayoishi....
Diamond Platnumz ni msanii ambaye yuko kwenye level za juu
kwenye kila kitu kwa sasa, upande wa muziki na hata aina ya maisha
anayoishi. Hilo linaweza kuthibitishwa na gharama zilizotumika
kufanikisha sherehe yake ya kutimiza miaka 25 iliyofanyika jana October
2, pamoja na zawadi aliyopewa na uongozi wake.
Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema party hiyo iligharimu shilingi milioni 28 na kuwataja waliohusika kuigharamia.
“Event tumefanya wenyewe lakini mwisho wa siku Diamond yupo karibu na watu wengi na makampuni mengi”. Tale ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “Coca
cola kama Coca Cola ndio walichukua nafasi kubwa kuifanya ile event
sababu wao ni balozi wao….ilikuwa gharama inagharimu milioni 28 kwa
sisi wenyewe watoto wa paka tusingeweza kuitoa kirahisi hiyo hela.”
Zawadi kubwa aliyopata Diamond kwenye birthday yake ni gari aina ya
BMW X6, ambayo alipewa na uongozi wake unaoundwa na Babu Tale, Said Fela
na Salam. Tale ameelezea jinsi walivyoweza kupata pesa za kununua gari
hiyo.
“Sasa hivi Diamond anafanya vizuri na tulikuwa tunamwambia
Diamond kwamba kuna contract tukisaini tutakupa zawadi, as in kwamba
management haitachukua percent ya hiyo contract hiyo pesa itaenda kwenye
kukuchukulia wewe zawadi, akasema nyie bana mlivyokuwa watata sijui
kama mtakubali.”
Aliendelea,
“Tulivyotoka South Africa tukawa kuna contract tume confirm
kusaini, tulivyosaini ile contract ile pesa ambayo ilitakiwa pasenti
yote ije kwetu sisi mimi, Fela na Salam yote tukasema tumchukulie
zawadi….ni shilingi ya kitanzania milioni 90”.