Muimbaji wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Tanzania, ametumia shilingi 700,000 za Kenya a...
Muimbaji wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee ambaye hivi
karibuni alikuwa nchini Tanzania, ametumia shilingi 700,000 za Kenya
ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 12 za Tanzania kuhudhuria hafla
mbili ikiwemo ya mwanae wa kike zilizofanyika siku moja.
Esther Akoth aka Akothee akiwa kwenye helikopta aliyokodi
Akothee ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Akothee Safaris: Tours & Travel ya Mombasa,
Kenya ameiambia Bongo5 kuwa imemlazimu kutumia gharama hiyo kwakuwa
hakutaka kukosa hafla hizo zilizofanyika leo katika miji tofauti,
Eldoret na Nairobi nchini humo.
“Sikuwa na namna lakini imenilazimu kuhudhuria hafla zote bila
kuumiza hisia za mwanangu Prudence Vanpelt ambaye yupo Utawala Academy
Nairobi na pia kukosa mahafali ya mdogo wangu Moi University, Eldoret,”
amesema.
“Bila kusahau kazi yangu na mapenzi katika muziki, natakiwa kurejea
Nairobi kesho (Jumamosi) kufungua show ya Chameleone kwenye party ya
huko Athi River, Nairobi.”
Akothee amesema rubani wa helikopta hiyo ndiye aliyembeba Akon wakati
akiwa Kenya. Mfahamu zaidi msanii huyo kwa interview aliyofanya na
Bongo5 hivi karibuni.