NAJUA, watu wengi wanakuambia ni lazima wawe na wivu kwa wenza wao kwa sababu hiyo ndiyo maana ya kupenda. Ninakubaliana nao, lakin...
NAJUA, watu wengi wanakuambia ni lazima wawe na wivu kwa wenza wao kwa sababu hiyo ndiyo maana ya kupenda. Ninakubaliana nao, lakini siungani nao. Niko tofauti, sitaki kuwa na wivu na nitajaribu kueleza kwa kadiri ninavyoweza ili uweze kunielewa.
Kule kwenye simu nako kwa mfano, mke au mume anapofuatilia sms na simu za mwenzake, mwisho wa siku ni kelele, ambazo kwa vyovyote hazina matokeo mazuri. Lakini kama mtu ataweka wivu mbali kwa mtu wake, anapunguza sehemu kubwa ya hatari ya ndoa au uhusiano wake kuvurugika. Jambo moja la msingi kukumbuka ni kwamba, kadiri mizozo na misuguano inavyokuwa mingi, ndivyo uwezekano wa kutengana unavyozidi. Kutokuwa na wivu hakumaanishi haupendi. Unampenda lakini unajitahidi kumpa nafasi ya yeye kukuheshimu. Watu wengine huamua kusaliti kwa sababu ya hasira, hufanya kama wanakomoa kwa sababu mtu unajijua hufanyi lolote, lakini mwenzako kila siku kelele. Kudumu kwa ndoa au uhusiano ni pamoja na kila mmoja kukubali kuamini juu ya nyendo za mwenza wake. Inapotokea umefumania, iwe ni bahati mbaya sana, ambayo hata aliyefumaniwa atajisikia vibaya, lakini siyo kufumania kwa kulazimisha. Ukiwa hujishughulishi naye kwa kiwango kile, hata yeye unampa wasiwasi, anakuwa mgumu kuamini kama unampenda kweli, hivyo atazidisha umakini ili asije akawa chanzo!