Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia kufanyika kwa tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Beer Fest’ lililokuwa l...
Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia
kufanyika kwa tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Beer Fest’ lililokuwa
linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.
Uamuzi wa mahakama hiyo umetokana na malalamiko yaliyotolewa na
Bongo5 Media Group ambao wanamiliki wazo halisi la tamasha la aina hiyo
liitwalo Dar es Salaam Beer Fest.
Kwa hali hiyo mahakama hiyo imetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa
‘Bang Bang Beer Fest’ lililokuwa lifanyike October 4 kwenye viwanja vya
Posta Kijitonyama, Dar es Salaam pamoja na kulipa hasara yoyote
iliyotokana na kuingiliwa kwa haki miliki hiyo.