MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha ka...
MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha katika tukio la kuchumbiwa kunaswa na mwenyewe kudai si yeye aliyechumbiwa.
Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata.
Kwa
mujibu wa chanzo, tukio hilo limedaiwa kufanyika kwa siri hivi karibuni
nyumbani kwa miss huyo, Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu wa
karibu.
“Inaonesha
hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu wengi siku hiyo, hata
hao ndugu wenyewe hawakuwa wengi kiivyo lakini picha zinaonesha
Flaviana akichumbiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi
kumwaga data chanzo hicho kilidai kwamba, mwanaume anayetaka kumuoa
mrembo huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ni Mchaga
mwenye fedha zake aishiye Marekani.
“Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.
“Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.
Flaviana Matata.
Amani
lilifanikiwa kuzinasa picha hizo ambazo zinamuonesha mrembo huyo akiwa
amepiga magoti huku amemshika mkono mmoja wa wazazi wake aliyeshiriki
katika hafla hiyo ya kupokea mahari.
Baada ya
kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Flaviana kwa njia ya simu ya
mkononi ndipo alipokataa katakata kuwa si yeye aliyekuwa akichumbiwa
bali ni dada yake.
“Hamna
kitu kama hicho, unayesema alikuwa anachumbiwa si mimi ni dada yangu,
mila za kwetu Shinyanga nalazimika mimi kumsindikiza hivyo kama umeona
picha hizo uelewe hivyo,” alisema Flaviana.
Hata
hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ni la Flaviana na
si dada yake hivyo kuzidi kuzua utata juu ya ukweli halisi, Amani
linaendelea kufatilia kwa karibu.