MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya penzi lake na msanii Maximilian Bushoke ku...

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya penzi lake na msanii Maximilian Bushoke kuwa na sarakasi nyingi lakini anaamini atamuoa.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Akizungumza na paparazi wetu, Jini alisema watu wengi wamekuwa
wakiuponda uhusiano wake kwa kuwa Bushoke anaishi Afrika Kusini na kuona
hakuna mapenzi ya kweli lakini ukweli anaoujua yeye ndoa ipo.
Msanii wa Bongo Fleva Maximilian Bushoke.
“Piga ua garagaza, Bushoke ndiye mwanaume ambaye anajua kunipa tiba
nzuri ya mapenzi, hakuna mwingine, atanioa tu kwa sababu sioni
kipingamizi,” alisema Jini Kabula