Msanii wa Hiphop Tanzania Afande Sele Afiwa na mama mtoto wake, Asubuhi ya kuamkia August 14 2014, Afande Sele aliweka ujumbe kuh...
Msanii wa Hiphop Tanzania Afande Sele Afiwa na mama mtoto wake,
Asubuhi ya kuamkia August 14 2014, Afande Sele aliweka ujumbe kuhusu
taarifa hizi “Ndugu
zangu!! Nimefiwa na Mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama
Tunda/Mama Sanaa) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. SISI NI WAJA WA
MWENYEZI MUNGU NA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA; MUNGU AMPUMZISHE PEMA.”
Ujumbe huu uliambatana na Hii picha ya familia yake.
Kabla ya kifo chake Afande alifarakana na mke wake na walikuwa
wakiishi sehemu tofauti, wana watoto wawili Tunda ambaye yuko kidato
cha pili na Sana mwenye miaka 2.
Msiba upo Morogoro Mtaa wa Amani kwa Wazazi Wa Asha mohamed Shengo.
Asha amezaliwa May 21 1981, Aliishi na Afande kwa miaka 16,Afande Sele
ameniambia Asha aliugua malaria siku moja kabla ya kifo chake.
Hisia za Mwananchi na Tabasam Blog Inatoa pole kwa Afande Sele na familia yake, Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amen