DAKTARI mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiri...
DAKTARI
mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa
na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni
mgonjwa aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa
utoto wake.
Nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa kuzungumzia tabia za
Shilole za kugombana mara kwa mara na mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama
zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia linalomsumbua mmoja wao au ni
ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.
“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa unyanyasaji akiwa mtoto ‘child
abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa, kupigwa, kunyimwa chakula au mateso
ya aina hiyo, akikua bila kupata tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo
kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu mzima.
“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kupenda kujitenga, hasira za
karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni kumfanyia mtu mwingine hasa
mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu wanaita ‘Propensity
Victimization,’” alisema daktari huyo.
Alisema katika nchi zilizoendelea, tatizo hilo hupewa kipaumbele
katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika kwani madhara
yake huwa ni pamoja na mwathirika kuamua kujinyonga au kuua.
Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana kufanana na matukio yaliyowahi
kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa miaka 14, aliwahi kubakwa, pia
anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu wenye umri mkubwa, ikiwa ni
pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri mdogo.