BONGE la Bwana, Jacob Stephen ‘JB’ amewaasa wasanii wa kike akiwataka wajitambue ili waweze kuishi kwa muda mrefu katika gemu la sanaa....
BONGE
la Bwana, Jacob Stephen ‘JB’ amewaasa wasanii wa kike akiwataka
wajitambue ili waweze kuishi kwa muda mrefu katika gemu la sanaa.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Wastara Juma.
“Nawasihi wasanii wengine wa kike kuiga maisha ya Wastara pamoja na
misukosuko ya maisha ya hapa na pale lakini bado anajitambua, anapigana
na kusimama, ujue wanawake muda wao ni mchache katika sanaa tofauti na
wanaume lakini kwa Wastara bado yuko,Happy birthday Wastara,’ alisema
JB.
Bonge la Bwana, Jacob Stephen ‘JB’.
Akizungumza katika sherehe ya kuzaliwa msanii Wastara Juma alisema,
wasanii wengi wa kike wana muda mchache sana kwenye tasnia ya sanaa, ila
kwa Wastara kajitahidi sana na bado anaendelea kuishi katika sanaa
kutokana na kujitambua kwake.