Stori: Makongoro Oging’ MMH! Majanga! Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Juliet G...
Stori: Makongoro Oging’ MMH!
Majanga! Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Juliet Gaison Komba (37),
mkazi wa Mbagala Kuu, Temeke, Dar hivi karibuni amekutwa na mauti akiwa
Gesti ya Kigoma, Mbagala Charambe, Dar.
Waombolezaji wakilia kwa unchungu kanisani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, mwanamke huyo ambaye mumewe ni
kigogo mwenye cheo cha mkurugenzi wa kampuni moja ya usafirishaji jijini
Dar, alikutwa na mauti baada ya kuingia kwenye gesti hiyo na mwanaume
mmoja aliyedaiwa kuwa ni hawara yake licha ya kuwa na mume.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo, Nickson John alisema siku ya tukio,
mwanamke huyo na jamaa yake aliyevaa kofia maarufu kwa jina la kapelo,
walifika kwenye gesti hiyo saa saba mchana.
Alisema: “Waliulizia chumba chao cha siku zote maana walikuwa wakifika kila wakati, nikawaambia kiko wazi.
Ndugu na jamaa wa karibu wakiomboleza msibani.
“Nilifuatana na mwanaume hadi kwenye chumba hicho namba 5, alilipia
kisha kuzama na huyo mwanamke.“Saa kumi mwanaume alitoka, akaniambia
anakwenda kutafuta chakula endapo mwanamke wake atahitaji kinywaji
nimpe.
“Ilipofika saa kumi na mbili jioni,
nilianza kuingiwa na hofu kwani yule mwanaume alikuwa hajarudi na
mwanamke hakutoka kuhitaji kinywaji.“Niliamua kwenda kugonga mlango
lakini hakuitika. Niliendelea kukaa kusubiri kama yule mwanaume atarudi
lakini wapi!
Padri akiweka msalaba juu ya kaburi la marehemu Juliet Gayton Komba.
“Saa moja usiku nikiwa sijawaona, nikaenda kugonga kwa nguvu huku
nikiita bila mafanikio, bosi wangu aliyelala chumba kingine alinisikia
akaja.“Nilimweleza tatizo naye aligonga hakuna aliyeitika, tukazunguka
dirishani kuchungulia, tukamwona mwanamke amelala kitandani lakini
tulipata wasiwasi huenda alipatwa na tatizo.
“Bosi wangu aliwapigia simu polisi, walifika na kuvunja mlango ambapo
walimkuta mwanamke amekufa huku akitokwa damu mdomoni, waliuchukua
mwili hadi Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa uchunguzi.”
Mume wa marehemu Bw. Deusi Komba.
Akaendelea: “Si mara yao ya kwanza kuja hapa, kwa mwezi waliweza kuja
hata mara tano. Yule mwanaume hadi namba yake ya simu alinipa, ninayo.”
Kwa upande wake, Deusi Komba ambaye ni mume wa marehemu alipoulizwa
kuhusu tukio hilo alikiri kutokea.Alisema asubuhi ya siku hiyo alimuacha
marehemu nyumbani na kwamba hakuwa na mpango wa kutoka lakini aliporudi
jioni hakumkuta na simu yake kila alipoipiga ilikuwa ikiita bila
kupokelewa.
Juliet Gaison Komba (37) .
Alisema ilibidi aende Kituo cha Polisi Maturubai kutoa taarifa na
ndipo alipoelezwa kuwa, mkewe huyo anayemsaka amekutwa amekufa
gesti.Marehemu huyo alizikwa Jumanne iliyopita katika Makaburi ya
Mbagala Kuu, Dar na ameacha watoto watatu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke, (pichani) alipoulizwa alikiri kutokea kwa tukio na kusema
uchunguzi unaendelea.