HUYU ANATAKA KUJUA Dayna wewe ni mwenyeji wa wapi? Nakukubali sana katika fani kwa ...
HUYU ANATAKA KUJUA
Dayna wewe ni mwenyeji wa wapi? Nakukubali sana katika fani kwa kukusikia, sijawahi kukuona, natamani sana nikuone. Selemani Alifa, Dar, 0718803204
DAYNA: Nimezaliwa Mwanza ila nimekulia Dodoma. Kuhusu kuniona karibu sana kwenye shoo zangu ndiyo njia rahisi ya kuniona.
Kila kizuri kinahitaji pongezi, kiukweli wewe ni mzuri na una mvuto, hivi unaepuka vipi vishawishi vya michepuko maana sijawahi kusikia skendo zako? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
DAYNA: Nashukuru sana, kuhusu vishawishi ni jinsi unavyojiweka japokuwa vipo vingi lakini namshukuru Mungu ananiwezesha kuvishinda.
KUIBIWA NYIMBO
Dayna unakuja vizuri kwenye fani, hongera, kama mwanamuziki wa Bongo Fleva unazungumziaje suala la wanamuziki kuibiana nyimbo maana mtu anaweza kujitungia mashairi yake kwa muda mrefu halafu ikatokea mwingine akamuibia na kuweka midundo mingine hata wewe yalikukuta kwa Diamond (Nasibu Abdul). Rocky, Moshi, 0715289337
DAYNA: Ukiwa unajiamini huwezi kuiba lakini kikubwa ninachoweza kusema wanamuziki tunatakiwa kujituma na kufanya kazi kwa nguvu na sasa hivi wizi siyo sana tangu nilipotangaza kuhusu Diamond watu wamekuwa na uoga. HISTORIA
Kwa ufupi mimi ni shabiki wako mkubwa, napenda kujua historia yako kielimu na kimaisha. Dr Steve, Dar, 0654202397
DAYNA: Mimi ni mzaliwa wa Mwanza, nimekulia Dodoma, nina elimu ya kidato cha nne, nilikuja Morogoro kuhangaika kimaisha na ndipo nilipotokea kimuziki, ni mama wa mtoto mmoja.
MUZIKI UNALIPA?
Dayna unazungumziaje muziki wetu wa Bongo Fleva bado unalipa au ndiyo umeshapoteza mwelekeo? Salim Liundi, Dar, 0659601205
DAYNA: Muziki unalipa na jinsi unavyojituma na kujua nini mashabiki wako wanataka ndiyo unavyolipa zaidi.
Dayna hivi una undugu na Godfrey Nyange Kaburu au Mangaza Nyange? Muddy Madiley, 0652672805
DAYNA: Hapana ni majina tu yanafanana.
YEYE NA DIAMOND VIPI?
Nakupenda sana dada, unafanya kazi vizuri hongera, hivi ulichukua uamuzi gani Diamond alipokuibia wimbo wako? Msomaji, Moshi, 0655806266
DAYNA: Nilihangaika sana nikifuatilia mpaka kwenye vyombo vya sheria lakini mwisho wa siku mimi ni mtoto wa Kiislamu niliamua kumwachia Mungu ndiyo maana naendelea vizuri na kazi ya muziki na nawashukuru ninyi mashabiki wangu kwa kunikubali.
SKENDO AMBAYO HATAISAHAU
Nakukubali sana Dayna, ni skendo gani iliyowahi kukupata ambayo hutaisahau maishani mwako? Msomaji, 0659868893
DAYNA: Sina skendo kubwa sana ila iliyoniumiza ni ile ya kwamba ninatoka na Mr Blue wakati nilikuwa nafanya naye kazi tu na namheshimu sana.
JINA LA MWANAYE
Dayna mwanao anaitwa nani na ana umri gani? Tima Mashi, Dar, 0654929309
DAYNA: Mwanangu anaitwa Rahma Nyange ana miaka nane.
SWALI
Nakupongeza sana Dayna kwa kazi zako nzuri ila kiukweli mimi huwa nakukubali sana, ulizaa ukiwa na miaka mingapi kwani bado unaonekana mdogo? Nakushauri kaza buti. Dayana Mada, Dar, 0755799720
DAYNA: Asante, ukweli nilizaa nikiwa na umri mdogo lakini siwezi kusema ni miaka mingapi maana nitakuwa nawahamasisha watoto waone ni sawa kuzaa wakiwa wadogo.
Nakujua vizuri Mwanaisha ulikuwa unakaa Chang’ombe, Dodoma na ulikuwa na boy friend anaitwa Amony. Irene, Dodoma, 0758589308
DAYNA: Ni kweli.
TUKIO AMBALO HATALISAHAU
Nakukubali sana dada Dayna, je, ni tukio gani hutalisahau katika fani ya muziki? Stephano, Tanga, 0713152125
DAYNA: Yapo mengi sana ila namshukuru Mungu ananipigania, nafanya kazi na mashabiki zangu mnanipokea.
Dayna wewe ni mwenyeji wa wapi? Nakukubali sana katika fani kwa kukusikia, sijawahi kukuona, natamani sana nikuone. Selemani Alifa, Dar, 0718803204
DAYNA: Nimezaliwa Mwanza ila nimekulia Dodoma. Kuhusu kuniona karibu sana kwenye shoo zangu ndiyo njia rahisi ya kuniona.
Mbongo Fleva, Dayna Nyange
MICHEPUKOKila kizuri kinahitaji pongezi, kiukweli wewe ni mzuri na una mvuto, hivi unaepuka vipi vishawishi vya michepuko maana sijawahi kusikia skendo zako? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
DAYNA: Nashukuru sana, kuhusu vishawishi ni jinsi unavyojiweka japokuwa vipo vingi lakini namshukuru Mungu ananiwezesha kuvishinda.
KUIBIWA NYIMBO
Dayna unakuja vizuri kwenye fani, hongera, kama mwanamuziki wa Bongo Fleva unazungumziaje suala la wanamuziki kuibiana nyimbo maana mtu anaweza kujitungia mashairi yake kwa muda mrefu halafu ikatokea mwingine akamuibia na kuweka midundo mingine hata wewe yalikukuta kwa Diamond (Nasibu Abdul). Rocky, Moshi, 0715289337
DAYNA: Ukiwa unajiamini huwezi kuiba lakini kikubwa ninachoweza kusema wanamuziki tunatakiwa kujituma na kufanya kazi kwa nguvu na sasa hivi wizi siyo sana tangu nilipotangaza kuhusu Diamond watu wamekuwa na uoga. HISTORIA
Kwa ufupi mimi ni shabiki wako mkubwa, napenda kujua historia yako kielimu na kimaisha. Dr Steve, Dar, 0654202397
DAYNA: Mimi ni mzaliwa wa Mwanza, nimekulia Dodoma, nina elimu ya kidato cha nne, nilikuja Morogoro kuhangaika kimaisha na ndipo nilipotokea kimuziki, ni mama wa mtoto mmoja.
MUZIKI UNALIPA?
Dayna unazungumziaje muziki wetu wa Bongo Fleva bado unalipa au ndiyo umeshapoteza mwelekeo? Salim Liundi, Dar, 0659601205
DAYNA: Muziki unalipa na jinsi unavyojituma na kujua nini mashabiki wako wanataka ndiyo unavyolipa zaidi.
Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue akipozi
UNDUGUDayna hivi una undugu na Godfrey Nyange Kaburu au Mangaza Nyange? Muddy Madiley, 0652672805
DAYNA: Hapana ni majina tu yanafanana.
YEYE NA DIAMOND VIPI?
Nakupenda sana dada, unafanya kazi vizuri hongera, hivi ulichukua uamuzi gani Diamond alipokuibia wimbo wako? Msomaji, Moshi, 0655806266
DAYNA: Nilihangaika sana nikifuatilia mpaka kwenye vyombo vya sheria lakini mwisho wa siku mimi ni mtoto wa Kiislamu niliamua kumwachia Mungu ndiyo maana naendelea vizuri na kazi ya muziki na nawashukuru ninyi mashabiki wangu kwa kunikubali.
SKENDO AMBAYO HATAISAHAU
Nakukubali sana Dayna, ni skendo gani iliyowahi kukupata ambayo hutaisahau maishani mwako? Msomaji, 0659868893
DAYNA: Sina skendo kubwa sana ila iliyoniumiza ni ile ya kwamba ninatoka na Mr Blue wakati nilikuwa nafanya naye kazi tu na namheshimu sana.
JINA LA MWANAYE
Dayna mwanao anaitwa nani na ana umri gani? Tima Mashi, Dar, 0654929309
DAYNA: Mwanangu anaitwa Rahma Nyange ana miaka nane.
SWALI
Nakupongeza sana Dayna kwa kazi zako nzuri ila kiukweli mimi huwa nakukubali sana, ulizaa ukiwa na miaka mingapi kwani bado unaonekana mdogo? Nakushauri kaza buti. Dayana Mada, Dar, 0755799720
DAYNA: Asante, ukweli nilizaa nikiwa na umri mdogo lakini siwezi kusema ni miaka mingapi maana nitakuwa nawahamasisha watoto waone ni sawa kuzaa wakiwa wadogo.
Dayna Nyange akipozi.
ANAMJUA?Nakujua vizuri Mwanaisha ulikuwa unakaa Chang’ombe, Dodoma na ulikuwa na boy friend anaitwa Amony. Irene, Dodoma, 0758589308