post-feature-image
HomeBurudani

BAADA YAKUACHIKA: ROSE NDAUKA AANGUSHA SHEREHE!

SIKU chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangu...

DIAMOND, YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SIKU YA MSANII DAR
MAINDA AMLILIA SHERRY MAGARI
PICHA ZA WASTARA ZA CHUMBANI GUMZO KOTE MTANDAONI ZICHEK HAPA


SIKU chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.
 
Msanii nyota wa filamu nchini, Jack wa Chuz akimtunza msanii mwenzake, Rose Ndauka
Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.
 
Msanii wa filamu nchini, Mayasa(kushoto) akitoa sapoti ya kufungua shampeni katika sherehe hiyo ya bethidei ya Rose Ndauka.
Katika pati hiyo kulikuwa na vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi, huku pia vyakula vya aina mbalimbali vikipatikana, kiasi kwamba hadi gazeti hili linaondoka, pombe na vyakula bado vilikuwepo.
Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
 
Msanii nyota wa filamu Bongo, Shamsa Ford naye pia alikuwepo.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.
 
Baadhi ya wasanii  wa filamu nchini na wageni waalikwa wakila na kunywa.
Kwa upande wake, Rose alisema: “Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo yote yako vyema kabisa.”
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: BAADA YAKUACHIKA: ROSE NDAUKA AANGUSHA SHEREHE!
BAADA YAKUACHIKA: ROSE NDAUKA AANGUSHA SHEREHE!
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIx-PcZN8sBoLqmBHli77l4rghZnS6S7sq45N5usHtjeudovJs6fDBGBQMbLq0BBIKCx_WcKRTVkToLbuZCJxlfTNVyUZtvXPm93JZuK0tmMZ6pNIscw82N09kJkknnS2UNMLoDkooL7c/s1600/IMG_0374.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIx-PcZN8sBoLqmBHli77l4rghZnS6S7sq45N5usHtjeudovJs6fDBGBQMbLq0BBIKCx_WcKRTVkToLbuZCJxlfTNVyUZtvXPm93JZuK0tmMZ6pNIscw82N09kJkknnS2UNMLoDkooL7c/s72-c/IMG_0374.JPG
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/baada-yakuachika-rose-ndauka-aangusha.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/baada-yakuachika-rose-ndauka-aangusha.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago