Zimepita siku kadhaa tangu picha za Wastara na Bond kusambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha wawili hao waki...
Zimepita
siku kadhaa tangu picha za Wastara na Bond kusambaa mitandaoni na
kwenye vyombo vya habari zikionesha wawili hao wakiwa kimahaba zaidi na
sasa Wastara Juma ameamua kufunguka rasmi.
Wastara
alisema “zile picha zote mnazoziona ni picha zimo ndani ya filamu ya
Uaminifu Dhaifu ambayo imetoka leo,filamu hiyo nimecheza tofauti na
filamu zote nilizocheza kipindi cha nyuma hivyo nimesikitika sana
watanzania kuzichukulia tofauti na kuziandikia habari bila kuongea na
mimi,naomba mnunue filamu yangu mtaona kilichomo ndani ni filamu nzuri
sana niamini mimi”
Kwenye filamu hiyo Wastara amecheza na wasanii
wengine kama vile Nsungu,bambo,bond na matumini,inasambazwa na
stepsentertainnment.
>