Msanii ‘Chris Brown’ ajisikia vibaya sana baada ya kuona Clip ya Girlfriend wake ambayo imetolewa na BET wakati akifanyiwa Interview n...
Msanii ‘Chris Brown’
ajisikia vibaya sana baada ya kuona Clip ya Girlfriend wake ambayo
imetolewa na BET wakati akifanyiwa Interview na “Just KeKe” kuhusu
maisha yake. Karrueche alitoa machozi na kulalamika kuwa msanii
‘Rihanna’ na Fans wake walimtesa sana baada ya kitendo cha wasanii hao
kurudia kwa muda baada ya kuachana. Alisema yeye sio msanii ni mtu wa
kawaida tu ambae alikutana na Chris Brown na kumpenda kama mtu wa
kawaida na hajawahi hata siku moja kujua ni jinsi gani maisha ya wasanii
yanavyokuwa, ila baada ya kitendo hicho Fans wa Rihanna walimrudia kwa
matusi na vitisho ambavyo vilimuumiza sana na kutokujua nini cha kufanya
katika maisha yake.
Imeripotiwa kuwa Chris Brown baada ya kuona clip hiyo ambayo pia
mwanadada Karrueche alitamka kuwa Rihanna ni msanii mkubwa kumpita Chris
Brown, lakini msanii hiyo hakuchukia kabisa kitendo ambacho kinaonyesha
mabadiliko makubwa sana kwa msanii huyo baada ya kitoka jela na zaidi
ya kusema kuwa amegundua kuwa hakuwa Boyfriend mzuri kwa kipindi hicho
na anajisikia vibaya sana kwa kitendo hicho kilichotokea na kumfanyia
mpenzi wake huyo. Vile vile amesema kuwa kitendo cha Karrueche kutamka
kuwa msanii Rihanna ni mkubwa kuliko yeye wala hakimsumbui na kinamfanya
aweze kuongeza juhudi kufanya kazi zaidi kuweza kuuza muziki wake na
kufanya show ili kufikia viwango vya juu kimuziki duniani.
Breezy ambae amekuwa akitumia sana “Blood Sings” kwa muda mrefu
katika usanii wake, hivi karibuni baadabya kutoka jela alitumia kiasi
cha $10,000 kwa kubadilisha rangi ‘Lamborghini’ yake moja kuwa blue
ambayo sio Blue kabisa inasemekana imekuwa “customised” kwa blue
aliyokua anaitaka yeye inayojulikana kama “Blue Sky”
Vile vile ameamua kubadilisha muonekano wake hata wa nywele na kuamua
kufanya style ya 1930 ambapo African American wengi wa nchini marekani
walikuwa wanatengeneza nywele zao na kuamua kuwa na kuonekano huo ambapo
vyombo vingi vya habari havijakubaliana nae kabisa kwa kusema
anajiharibia image yake ambayo inapendwa sana na Fans wake