Baada ya kudai kunyimwa nafasi ya kupewa tuzo na waandaji wa tuzo mbalimbali nchini, H.Baba na mke wake Flora M...
Baada ya kudai kunyimwa nafasi ya kupewa tuzo na waandaji wa
tuzo mbalimbali nchini, H.Baba na mke wake Flora Mvungi, Jumamosi hii
ndani ya hoteli ya Giraffe Ocean View wanatajia kupeana tuzo wao kwa
wao.
Akizungumza, H.Baba amesema kuna mashabiki wao wengi wanapenda kuwaona wakipewa tuzo hali ambayo haijawahi kutokea.
“Hizi ni tuzo za kifamilia ambazo sisi tumeamua kupeana,” amesema.
“Mke wangu mimi ni mwigizaji mzuri sana na mashabiki wengi wanampenda na
wanajua uwezo wake katika tasnia ya filamu na mke wangu anatambua
mchango wa H.Baba katika jukwaa, mambo ya performance na yeye kaamua
kutoa ya kwake kwangu mimi.”
“Kwahiyo ni tuzo za wasanii lakini za kifamilia. Tunataka watu waone
kwamba mashabiki wanahitaji waone watu wao wakipewa hivyo vitu lakini
huwa hawapewi , sasa watu wanaamua kupeana wao kwa wao,” alisema H.
Baba.