post-feature-image
HomeBurudani

DOKII AMPA ASKARI RUSHWA YA BUSU

Stori: Sifael Paul /Global Publishers MAKUBWA, madogo yana nafuu! Mwigizaji wa kitambo na mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya...

SHILOLE AMCHAPA KOFI MCHUMBA WAKE NUH MZIWANDA
MBUZI WAZIBWA MIDOMO
OMMY DIMPOZ, IDRIS WAWALIZA WALIMU WA SHULE YA MBEZI, KIMARA


Stori: Sifael Paul /Global Publishers
MAKUBWA, madogo yana nafuu! Mwigizaji wa kitambo na mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya, Ummy Wenslaus 'Dokii' anadaiwa kutoa kali ya karne baada ya kumpa askari wa jiji rushwa ya busu, Ijumaa lina mkanda kamili.
 
Mwigizaji wa kitambo na mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya, Ummy Wenslaus 'Dokii' akiomba ruksa ya kusepa na gari kutoka kwa askari wa jiji (city parking).
Tukio hilo ambalo gazeti hili lina picha za mnato na video lilijiri kwenye Makutano ya Mtaa wa Narung’ombe na Swahili, Kariakoo jijini Dar, asubuhi ya saa 4:00, Septemba 15, mwaka huu.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu, Dokii alipaki ‘vibaya’ gari alilokuwa nalo aina ya Toyoya Noah la rangi nyeusi ambapo alifuatwa na kuambiwa kwamba sehemu aliyopaki hairuhusiwi.
Ilisemekana kwamba alitumia ‘ustaa’ wake kuwapuuza akaingia kwenye maduka na kuendelea na ‘shopping’ zake.Ilidaiwa kwamba aliporudi na kutaka kuondoka, alikuta mkoko huo umefungwa mnyororo na vyuma kwenye tairi la nyuma na askari wa jiji (city parking) hivyo akashindwa kutimua.
 
'Dokii' akitoa rushwa ya busu kumlainisha 'askari wa city'.
Ilielezwa kwamba baadaye alifuatwa na mkuu wa askari hao almaarufu kwa jina la Masai ambaye alimwambia kuwa alitakiwa kutoa faini ya shilingi elfu hamsini.
Iliendelea kudaiwa kwamba huku akidhani watu hawamjui alilianzisha na askari hao na kuanza kuzozana.
Muda mfupi baadaye ilijitokeza kadamnasi ambayo ilikuwa ikimzomea ndipo akakimbilia dukani kwa mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Chid.
 
'Dokii' akitoa namba ya simu kumlainisha askari huyo.
Ilidaiwa kwamba mwanaume huyo alimpatia msanii huyo shilingi elfu tano ili awapoze askari hao huku akimuombea wamfungulie gari aondoke lakini jamaa hao waliikataa.
Ilielezwa kwamba baada ya kuomba sana askari hao walikubali kumwachia baada ya kummwagia kiongozi wao mabusu ya kimahaba hadharani, kisa tu hakuwa na fedha ya kulipa faini.
Ilidaiwa kwamba baada ya kumlainisha jamaa huyo kwa mabusu motomoto na kufutiwa shitaka, aliachiwa huru bila kutoa chochote huku askari aliyeonjeshwa ‘utamu’ akibaki na mfadhaiko huku akiomba namba ya simu.
 
Askari wa 'city' akimruhusu 'Dokii' kuondoka eneo la tukio  mara baada kuchukua namba ya simu.
Ilisemekana kwamba ili kuua msala, msanii huyo alimpatia namba ya simu kisha akatoka nduki.
Ni rushwa? Kutoa kitu ili kununua haki kama alivyofanya Dokii ya kutoa busu ili aachiwe, nayo ni rushwa pia.Jitihada za kumpata Dokii ili kuzungumzia mkasa huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea. Stay tune!
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: DOKII AMPA ASKARI RUSHWA YA BUSU
DOKII AMPA ASKARI RUSHWA YA BUSU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8q2Xss5MiiRWEWBSaWuiQoNeKW9sB118nFvyAwF4PfxQn6k1GSgQWNzkOSyfT8VM9KjBp34j-TdLDgVvHkp5p-2NQ4ZtKhOI5emDiP3YLJbRoSoQOjt-WiUtFzbQhBQ6BeH3K37tv6BU/s640/DOKII.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8q2Xss5MiiRWEWBSaWuiQoNeKW9sB118nFvyAwF4PfxQn6k1GSgQWNzkOSyfT8VM9KjBp34j-TdLDgVvHkp5p-2NQ4ZtKhOI5emDiP3YLJbRoSoQOjt-WiUtFzbQhBQ6BeH3K37tv6BU/s72-c/DOKII.JPG
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/dokii-ampa-askari-rushwa-ya-busu.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/dokii-ampa-askari-rushwa-ya-busu.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago