Jengo likiungua na kudaiwa ndiyo la Hoteli ya Naura ya Arusha Jengo halisi la...
Jengo likiungua na kudaiwa ndiyo la Hoteli ya Naura ya Arusha
Jengo halisi la Naura Spring Hotel na kama lilivyo hada sasa.
Habari na picha zilizosambaa jioni hii kuwa Hoteli ya Naura Spring ya
jijini Arusha inaungua ni za uzushi. Akiongea na wanahabari jioni hii,
Meneja wa Hoteli hiyo iliyodaiwa kuongea, Bi. Beatrice Dallas, amesema
kuwa habari hizo zimesababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wake kwani
hakukuwa na tukio lolote la moto katika hoteli yake, hali ambayo
alijionea mwandishi wetu na kuchukua picha. Haikuweza kujulikana mara
moja ni mtu gani aliyesambaza taarifa na picha hizo za uongo kwenye
mitandao ya kijamii. Mtandao huu, ambao ulitumiwa picha na moja ya
wasomaji wake na kuiweka, unachukua nafasi hii kuwaomba radhi wale wote
waliopata usumbufu kwa tukio hili la kutengenezwa.