Kampuni ya ndege ya Korea imesema itasitisha safari za ndege zake kwenda nchini Kenya kuanzia Agosti 20 Kufuatia hofu ya kuenea kwa ugo...
Kampuni ya ndege ya Korea imesema itasitisha safari za ndege
zake kwenda nchini Kenya kuanzia Agosti 20 Kufuatia hofu ya kuenea kwa
ugonjwa wa Ebola.
Korean Air Lines Co Ltd imesema kuwa ndege zake zimekuwa zikifanya
safari mara tatu kwa wiki kutoka Incheon, Korea Kusini kwenda Nairobi.
Hatua hiyo imekuja baada ya shirika la afya duniani kutahadharisha
kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola
kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku
wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Source: Reuters/BBC Swahili