FUNGUKA! Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi ambaye ni mke wa ndoa wa msanii w...
FUNGUKA!
Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi ambaye ni mke wa ndoa wa msanii
wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ amefunguka kwamba
mwaka huu ameshindwa kufunga Mwezi Mtukufu (ukobe) kwa sababu
ananyonyesha.
Akijibu minong’ono ya watu iliyohoji kwa nini hafungi, Flora alisema
kutokana na mwanaye kuwa mchanga na kila mara anataka kunyonya,
ameshindwa kufunga kwani imekuwa vigumu kutokana na kupatwa na njaa ya
mara kwa mara.
“Jamani ngoja tu nimnyonyeshe mwanangu maana bado mdogo na mimi ni
mzazi hivyo sikuweza kufunga, ninatakiwa nile kila wakati kwa sababu
mwanangu ananyonya sana, msinitafsiri vibaya,” alisema Flora ambaye
amekuwa kibonge kupindukia.