Omarion akamatwa na kutiwa ndani leo baada ya kupita STOP sign bilankujali alama hiyo ya barabarani. TMZ wameripoti muda mfupi kuwa, t...
Omarion akamatwa na
kutiwa ndani leo baada ya kupita STOP sign bilankujali alama hiyo ya
barabarani. TMZ wameripoti muda mfupi kuwa, taarifa kutoka katika chanzo
chao cha habari ndani ya jeshi la police kuwa baada ya msanii huyo
kupita alama hiyo alisimamishwa na police, alipigwa pingu baada ya
police huyo kucheki leseni yake kwenye system na kukuta taarifa ya
‘arrest’ kutoka mahakani baada ya kusharau amri ya mahakama alipoitwa
kizimbani kwa kosa la kupewa ticket kwa uendeshaji mbaya alioufanya siku
za nyuma. Msanii huyo alipigwa pingu na kutiwa jela kwa muda na baadae
kuachiwa huru kwa dhamana ya dola za kimarekani $20,000.