KAULI ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuwa kiasi cha shilingi milioni 10 alizotoa haraka ...
KAULI ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuwa kiasi cha shilingi milioni 10
alizotoa haraka kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow alizowekewa na
mfanyabiashara James Rugemalila zilikuwa ni za mboga, zimewakera mastaa
kiasi cha kumshambulia na kumuita mwenye dharau iliyopitiliza.
Walisema
kauli hiyo inaonyesha jeuri waliyonayo watumishi wa umma, ambao hupata
fedha nyingi kwa njia zisizo halali kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru.
Mastaa hao ni pamoja na Baby Madaha, Nisha, Thea, Isabela, Tiko na
Amanda Poshi.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Tamlina Posh 'Amanda'.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar kwa njia ya simu,
walisema fedha hizo ni nyingi ambazo zingeweza kuwasaidia wagonjwa
mbalimbali, uchimbaji wa visima, kusaidia elimu, chakula kwa familia
zisizojiweza na makundi mengi yenye uhitaji.