KUTOKA moyoni? Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote amekuwa akimuombea dua shosti wake, Wema Sep...

KUTOKA moyoni? Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote amekuwa akimuombea dua shosti wake, Wema Sepetu ‘Madam’ na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ uhusiano wao udumu.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekie l(kulia) akiwa na shosti yake Wema sepetu.
Aunt alifunguka hayo mara baada ya kuulizwa na mwanahabari wetu juu
ya mtazamo wake kuhusu mapenzi ya wawili hao ambapo alisema mapenzi yao
yamekuwa yakimvutia na kila mmoja anaonekana kuwa na mapenzi ya kweli
kwa mwenzake hivyo hawezi kupendezwa hata siku moja akiona hawapo
pamoja.“Kusema kweli naona hawa watu wanapendana na kujaliana sana, siku zote nawaombea kwa Mungu mapenzi yao yadumu milele na ninaamini watafikia malengo yao, sitapenda hata siku moja kuona wapo tofauti,” alisema Aunt.
CREDIT; GPL