MSANII anayezidi kuja kwa kasi Bongo Movies, Happy Nyatawe ‘Suzy’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa kutokana na migogoro mb...
MSANII anayezidi kuja kwa kasi Bongo Movies, Happy Nyatawe ‘Suzy’ ametoa
kali ya mwaka baada ya kusema kuwa kutokana na migogoro mbalimbali
iliyokuwepo ndani ya Kundi la Bongo Movie, hata akipita njiani akiitwa
kwa kutumia jina hilo hatogeuka.
Msanii anayezidi kuja kwa kasi Bongo Movies, Happy Nyatawe ‘Suzy’ akipozi.
Suzy
alisema kutokana na ‘majanga’ kuwa mengi kundini, imefika hatua anaona
hata aibu kujitambulisha kuwa yeye ni msanii kutoka Kundi la Bongo
Movies.
“Kweli kabisa, mimi nikiitwa tu msanii wa Bongo Movie nikiwa napita njiani, sigeuki ng’o wataita mpaka wachoke kabisa, hali ni mbaya Bongo Movie tubadilike,” alisema Suzy.
“Kweli kabisa, mimi nikiitwa tu msanii wa Bongo Movie nikiwa napita njiani, sigeuki ng’o wataita mpaka wachoke kabisa, hali ni mbaya Bongo Movie tubadilike,” alisema Suzy.