post-feature-image
HomeBurudani

WEMA KORTINI TENA! KIFUNGO KIPO NJE NJE

Mkono wa sheria! Achana na drama zake na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mcheza sinema ‘grade one’ Bongo,...

JINI KABULA: PIGA UA BUSHOKE ANANIOA
WEMA NA DAU LA MILIONI ATAKAYEMUONA MBWA WAKE
BINTI ANYWA SUMU BAADA YA KUTOSWA NA MSANII WA BONGO FLAVA
Mkono wa sheria! Achana na drama zake na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mcheza sinema ‘grade one’ Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anapandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri, wakazi wa jijini Dar.


Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

HAYUKO PEKE YAKE
Katika kujibu kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.



KESI YENYEWE NI IPI?
Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya kazi na staa wa huko, Van Vicker, Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na Juma, tukio ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, Petit Man alipoteza simu na kuwahisi vijana hao ambao mmoja wao alikuwa ni fundi bomba, ambaye alikuwa akitengeneza bomba nyumbani hapo.


Mmoja wa vijana walioshambuliwa kwa kipigo nyumbani kwa wema.

WALIVYOWA-TEMBEZEA KICHAPO
Baada ya kuwabana vijana hao na kutotoshelezwa na majibu yao, ilidaiwa kwamba Petit Man, kwa kushirikiana na Wema waliwaita vijana wa kihuni ‘mbwa mwitu’ na kuwafungia nyumbani kwa Wema kisha kuwapa kipondo ‘hevi’ ili watoe simu hiyo lakini hadi dakika za mwisho walikataa kuwa hawakuchukua.

WASHITAKI MABATINI
Ilifahamika kwamba walipoachiwa baada ya kusulubiwa, vijana hao, wakiwa na majeraha, walikimbilia Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini na kufungua jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 SHAMBULIO 
LA KUDHURU MWILI.
Hata hivyo Wema na Petit walikamatwa na kuachiwa kwa dhamana kisha walisafiri nje ya nchi.


Petit Man.

KESI KUUNGURUMA LEO
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya mahakama hiyo, Wema na Petit Man watakuwa kizimbani asubuhi ya leo, kujibu mashtaka yanayowakabili ya kuwasulubu kwa kipigo cha mbwa mwizi vijana hao wawili.

“Wema na Petit Man watapandishwa kizimbani Jumatatu (leo), kesi imewakalia vibaya, kifungo njenje katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni tayari kwa kujibu kesi ya shambulio la kudhuru mwili kwa mujibu wa shitaka lililofunguliwa kituoni hapo.

“Kimsingi Wema kaponzwa na huyo Petit Man na ukizingatia tukio lenyewe lilifanyika nyumbani kwake.
“Hapo kesi ya Wema itakuwa ni kuthibitisha kama kweli tukio lilitokea nyumbani kwake siku hiyo na kwa nini aliamua kuruhusu ukiukwaji wa sheria kutokea nyumbani hapo wakati yeye kama mkuu wa familia alikuwepo na hakutoa taarifa ya aina yoyote kwenye mamlaka ya juu ya serikali,” kilidai  chanzo chetu.
Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zilieleza kuwa bado Wema na Petit Man walikuwa hawajatua Bongo.

Siyo mara ya kwanza kwa Wema kufikishwa mahakamani kwani aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya kumpiga mtu na ile ya kuvunja vioo vya gari la aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu  Steven Kanumba.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: WEMA KORTINI TENA! KIFUNGO KIPO NJE NJE
WEMA KORTINI TENA! KIFUNGO KIPO NJE NJE
http://api.ning.com/files/1D30FS3uScu7QRIIwUnZf-MZGMh2qCz7AazTRF6chdt-AR3WJI7AW7Cj*dyvGwQIRYRxT3mMwTbERjmfpS8qJjKWz0kQirRM/UdakuSpecially..jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/wema-kortini-tena-kifungo-kipo-nje-nje.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/wema-kortini-tena-kifungo-kipo-nje-nje.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago