Miss Tanzania wa zamani, Happiness Millen Magese alijikuta kwenye wakati mgumu wakati akihojiwa na Global TV kuhusu tatizo la En...
Miss Tanzania wa zamani, Happiness Millen Magese alijikuta
kwenye wakati mgumu wakati akihojiwa na Global TV kuhusu tatizo la
Endometriosis lilimfanya afanyiwe upasuaji mara 12 na na hivyo kuwa
mgumba.
Hali hiyo ndio imemlazimu mwanamitindo huyo kuanzisha taasisi ya
kuwasaidia wanawake wengine hapa nchini ili waepuke kile ambacho
kimemkuta yeye baada ya kuondolewa kizazi.
Kwenye mahojiano hayo, Millen amedai kuwa aliamua kutoa kizazi chake
ili aje kuasili (adopt) mtoto atakayemlea kama wake kwakuwa hakupenda
kujaribu kuzaa kawaida kwakuwa angempa tatizo hilo mwanae kama angezaa
wa kike.