Stori: Laurent Samatta ULE uchumba wa muda mrefu wa mwanadada aliyewahi kuwa Miss R...
Stori: Laurent Samatta ULE
uchumba wa muda mrefu wa mwanadada aliyewahi kuwa Miss Ruvuma miaka ya
nyuma, Isabela Mpanda ‘Bela’ na mwanamuzi Luteni Karama, upo kwenye
hatihati ya kuvunjika kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kitendo cha usagaji
anachoendelea kukifanya Bela anapokuwa na Baby Madaha.
Miss Ruvuma miaka ya nyuma, Isabela Mpanda ‘Bela’ akiwa na Baby madaha.
Akizungumza na paparazi wetu Bela alisema, licha ya kuzungumza mara
kwa mara na Karama kwamba kaacha tabia hiyo lakini hamuelewi.“Sifanyi
mambo hayo na kama watu bado wanaamini hivyo si kweli kwa sababu kitendo
hicho ndiyo kimesababisha hadi uchumba wangu na Karama uwe mashakani,”
alisema Bela.
Alipotafutwa Madaha ili kusikia kauli
yake kufuatia madai hayo alisema yeye na Bela ni marafiki wa muda mrefu
na kwamba masuala ya usagaji hataki hata kuyasikia maishani mwake.
Bela na Baby madaha wakipozi kimahaba.
“Sina muda wa kuvunja uchumba wa Karama na Bela na kitendo cha
usagaji kwangu sitaki hata kukisikia,” alisema Baby Madaha na kuongea:
“Kama wanataka kuachana basi wasitumie njia hiyo ili mimi nionekane
mbaya mbele za watu.”