post-feature-image
HomeBurudani

MKONGO WA WOLPER, HUSNA: NAMTAKA LULU KWA GHARAMA YOYOTE!

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong...

Haya Ndio Maneno ya Peter Manyika kuhusu tuhuma za kumtelekeza mama yake mzazi.
Heka heka leo Hii Ni Kuhusu Mke aliyeamua kwenda kumfumania Mumewe #HEKAHEKA
’Najitahidi Kumfurahisha Diamond’ - Wema Sepetu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu ‘Mkongo’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.
Mwami Rajabu ‘Mkongo’.
Akizoza na gazeti hili ndani ya Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar, mapema wiki hii, Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo.
“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper, Husna mara Wema, si kweli, hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi (Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu,” alisema Mwami bila soni.
Mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake.
“Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana,” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea.
Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar, hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MKONGO WA WOLPER, HUSNA: NAMTAKA LULU KWA GHARAMA YOYOTE!
MKONGO WA WOLPER, HUSNA: NAMTAKA LULU KWA GHARAMA YOYOTE!
http://api.ning.com:80/files/eOkD9SMZvVpPTSGxgBE-XF6KiBIiZDRsiC-7dIr-2iTfUxLzWvc8D2ec*5LnqurYr1FZg69lMmXOabdC5jxT32jQ6dLo7yV7/IMG20140325WA0004.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mkongo-wa-wolper-husna-namtaka-lulu-kwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mkongo-wa-wolper-husna-namtaka-lulu-kwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago