BAADA ya mwanamuziki Tiko Hassan kupokea kipigo kutoka kwa bwana wake aliyefahamik...
BAADA
ya mwanamuziki Tiko Hassan kupokea kipigo kutoka kwa bwana wake
aliyefahamika kwa jina moja la Ally, msanii huyo amesema hawezi kumuacha
kwani anampenda.
Mwanamuziki Tiko Hassan wakati akiuguza majeraha ya kipigo kutoka kwa bwana wake.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Tiko alisema ni kweli ameumizwa
kichwani lakini hawezi kufanya uamuzi wa kumuacha kwa kuwa, anahisi kuna
siku atajutia uamuzi wake huo.
“Ni kweli amenifanyia kitendo kibaya, ameniumiza lakini najua ni
hasira tu, hata yeye mwenyewe najua anajutia hivyo siwezi kumuacha,”
alisema Tiko ambaye alijiingiza kwenye filamu lakini sasa kageukia
muziki na anakuja na ngoma yake iitwayo Funga Virago.