STAA wa Pop Rihanna usiku wa kuamkia juzi aliungana na wachezaji wa Ujerumani kusherehekea ubingwa wao wa Kombe la Dunia baad...

STAA wa Pop Rihanna usiku wa kuamkia juzi aliungana na wachezaji wa
Ujerumani kusherehekea ubingwa wao wa Kombe la Dunia baada ya ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Argentina nchini Brazil.
Staa huyo aliyeonyesha mahaba dhahiri na timu hiyo ya Ujerumani akiwa
ameshika jezi ya timu hiyo, alishindwa kuvumilia baada ya Mario Gotze
kufunga bao katika dakika ya 113 ambapo aliamua kuvua nguo yake
aliyokuwa amevaa na kuonyesha brazia yake.
Baada ya mtanange huo, Rihanna aliungana na wachezaji katika hafla ya
kusherehekea ubingwa huo ambapo alipata fursa ya kupiga picha na
wachezaji pamoja na kombe hilo.