post-feature-image
HomeBurudani

KIGOGO WA UNGA AHENYESHWA POLISI

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mh...

LULU AHIFADHI NGUVU ZA KUJIFUNGUA
KADJA NITO MSANII NYOTA WA KIZAZI KIPYA HUU NDIO MUONEKANO WAKE KWA SASA.PICHA ZAIDI ZIKO HAPA.
WAPENZI WADONDOKA TOKA GHOROFA YA 6 WAKIFANYA YAO NA KUFARIKI DUNIA!
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’ mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.
Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.
Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.
Christina Naphtali Kigaye akiwa katika kituo cha polisi.
Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya  Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.
“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.
“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
“Alihojiwa kwa saa nyingi hadi akatokwa na jasho, maswali yalikuwa mazito,” alisema mtoa taarifa wetu.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: KIGOGO WA UNGA AHENYESHWA POLISI
KIGOGO WA UNGA AHENYESHWA POLISI
http://api.ning.com:80/files/06WphArD*Mt8Y0*ttnk4-268f8YyyCZXfQyyzki9VLLtOSPwCpXVnU7w08rQS*wb1zFZ0-cbCcuuAV4lAwcxsqO9MPqEwhlX/IMG_1354.JPG?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/kigogo-wa-unga-ahenyeshwa-polisi.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/11/kigogo-wa-unga-ahenyeshwa-polisi.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago