MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kw...
MASTAA wana mambo! Mtoto
mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake
kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu
yanapoteza muda bila sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi pale
atakapokuwa akijifungua.Mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu, Lulu alisema siku hizi
wanaume wengi wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea penzi kutokana
na migogoro isiyokuwa na msingi.“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema Lulu.