MWANAMUZIKI mkali wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amedaiwa tena kuhusika katika utapeli wa shilingi milioni mbili. Muandaaji ...
MWANAMUZIKI mkali wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amedaiwa tena kuhusika katika utapeli wa shilingi milioni mbili.
“Huu ni utapeli wa hali ya juu, maana alipewa pesa yote ya shoo, cha kushangaza hakutoa taarifa yoyote ya dharura, simu akipigiwa hapokei na wala meseji hajibu,” alisema Ibrahim.
Rose alipopigiwa simu ili kujua madai hayo kama yana ukweli, simu yake iliita bila ya kupokelewa hivyo akatumiwa meseji ambayo nayo ilionesha kumfikia lakini hakujibu chochote.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
Hivi karibuni, Rose alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja
aliyopewa kama malipo ya kutumbuiza katika uzinduzi wa albamu ya
mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.(CREDIT: GPL)