WASANII wa filamu nchini, Bond Bin Sinan na Salim Ahmed ‘Gabo’ hivi karibuni walinaswa wakisaga mirungi hadharani bila kujali kadamnasi...
WASANII
wa filamu nchini, Bond Bin Sinan na Salim Ahmed ‘Gabo’ hivi karibuni
walinaswa wakisaga mirungi hadharani bila kujali kadamnasi.
Gabo aking'ata mirungi.
“Duh! Jamani hawa wasanii wanakula mirungi hapa ukumbini ambako kuna
watu kibao na wa aina mbalimbali hawaoni kwamba wanavunja sheria za
nchi?” alisikika mmoja wa waalikwa.
Wenyewe walipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, hawakuwa tayari kujibu lolote zaidi ya kuendelea kutafuna.
Meza ya wasanii wa filamu Gabo na Bond ikiwa na dozi ya kutosha ya mirungi.
Ishu hiyo ilitokea katika Ukumbi wa Dar West, Tabata Dar kulikokuwa
na sherehe ya bethdei ya Wastara Juma ambapo wasanii hao walikuwa
wamejaza mirungi kwenye mfuko wa nailoni na kuweka mezani huku
wakitafuna kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shughuli.Wenyewe walipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, hawakuwa tayari kujibu lolote zaidi ya kuendelea kutafuna.