Habari zilizozagaa mitaani kupitia mtandao wa Instagram kuwa staa wa filamu za Kibongo Aunt Ezekiel huenda ni mjamzito, zimekanushwa na ...
Habari zilizozagaa mitaani kupitia mtandao wa Instagram kuwa
staa wa filamu za Kibongo Aunt Ezekiel huenda ni mjamzito, zimekanushwa
na muigizaji huyo.
Alipoulizwa kupitia U Heard ya XXL ya Clouds Fm kama anatarajia kuwa
mama, Aunt amesema hana ujauzito wowote isipokuwa anachojua yeye
amenenepa tu na kama mimbo ipo basi watu wataona. Baadhi ya mashabiki
wake wamekuwa wakimuuliza kama ni mjamzito kutokana na muonekano wa
tumbo lake kwa sasa.
Pia Aunt amekanusha kuwa na uhusiano na dancer wa Diamond aitwaye Moze Iyobo.