Ukweli haufichiki daima labda kuuchelewesha tu! Ndicho kinachomkuta muigizaji wa kike wa filamu ya ‘Django Unchained’ wa...
Ukweli haufichiki daima labda kuuchelewesha tu! Ndicho kinachomkuta muigizaji wa kike wa filamu ya ‘Django Unchained’ wa Marekani, Daniele Watts aliyewapa wakati mgumu polisi wa Los Angeles kwa kuwatuhumu kumnyanyasa na kumfanyia ubaguzi wa rangi alipokuwa na mpenzi wake Brian James.
Awali Daniele alisababisha matatizo kwa polisi hao baada ya kuonekana
katika picha akiwa analia mbele ya polisi hali iliyoaminika kuwa
alikuwa anaonewa.
Lakini TMZ wamepata picha na ushahidi kutoka kwa shuhuda wa tukio
hilo ambaye ameeleza kuwa aliwaona Daniele na mpenzi wake Brian wakiwa
katika harakati za kufanya mapenzi kwenye gari.
Picha hizo zilizochukuliwa katika eneo la tukio siku ya Alhamisi
zinaomuonesha Daniele na Brian wakiwa wameegesha gari, mlango mmoja
ukiwa wazi wakifanya kilichokatazwa kisheria.
Inaelezwa kuwa mtu mmoja aliyeliona tukio hilo aliwaita polisi na kila kitu kiliwekwa wazi muda huo.
Katika sauti iliyonaswa na TMZ, muigizaji huyo anasikika akiwasumbua
polisi hao kwa maneno na kutumia 'F-Word' kwenye sentensi zake.
Katika sauti nyingine iliyonaswa na Mail Online, Daniele anasikika
akimwambia polisi aliyemfunga pingu kuwa anajua haki zake kutokana na
uzoefu alioupata katika uigizaji.
Daniele Watts alicheza uhusika wa poliso katika comedy ya ‘Weeds’ ya mwaka 2012.