Archive Pages Design$type=blogging

MAAJABU MWANAUME APATA SIKU KAMA WANAWAKE

MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina  la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jiji...


MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina  la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia ya haja kubwa.


Frank Kalamu akiombewa kanisani.

Akitoa ushuhuda huo ndani ya Kanisa la The Revelation lililopo Buza-Kipera Desemba 21 mwaka huu, Frank alidai amepata mateso hayo kwa muda mrefu huku akizunguka kwa waganga na madaktari wengi bila mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho ameshindwa kushiriki tendo la ndoa na mkewe.

Akizungumza na waandishi wetu nje ya kanisa, Frank alisema awali alikuwa mzima lakini ghafla alianza kwa kukosa hamu ya kushiriki tendo na mkewe, ingawa alipojaribu kuchepuka, alimudu vyema kazi hiyo.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.


...Frank Kalamu akizidi kupokea upako.

“Nikawa nikijisaidia kitu kama utumbo unatoka, huku damu zikitoka pia, siku nyingine japokuwa ‘sikubleed’ lakini nyama hiyo ilitoka na nikawa nairudishia kwa ndani,” alisema Frank  kwa uchungu na kuongeza kuwa alianza kuhangaika kwa waganga mbalimbali bila msaada wowote.

Baada ya kuona anamaliza fedha bila kupata nafuu, Frank aliamua kutafuta huduma ya kiroho ambapo akiwa kanisani hapo, Nabii Yaspi alimwambia kuwa alikuwa amerogwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Saidi, ambaye mgonjwa huyo alimtambua kama rafiki yake wa zamani aliyewahi kumhisi kuwa alitembea na mchumba wake.


...akitoa ushuhuda wake.

“Nabii aliponiambia kuwa ni Saidi aliyeniroga, picha ya rafiki yangu ilikuja kichwani, kila mara alinihisi natembea na mchumba wake. Nadhani aliniroga kwa sababu hiyo si nyingine,” alisema mtu huyo ambaye pia alidai kufuatia huduma ya maombezi anayoipata, anaanza kuona dalili za mabadiliko ya hali yake.

 CHANZO:GPL

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MAAJABU MWANAUME APATA SIKU KAMA WANAWAKE
MAAJABU MWANAUME APATA SIKU KAMA WANAWAKE
http://api.ning.com/files/BybgAqvu3OnyoJwumxuXWGEMSokVxtq4uYElptVe7HJaGe1Sldo9wDrORoei98ToNeRC*g9JbfJgrwFr4fsnbDFXEwFYtvPz/IMG_0227.jpg?width=650
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/maajabu-mwanaume-apata-siku-kama.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/12/maajabu-mwanaume-apata-siku-kama.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago