MSANII nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita alina...
MSANII nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita alinaswa Live akiwa kwenye pozi la aina yake akiwa na pedeshee maarufu jijini Dar anayefahamika kama Papaa Daudi ambaye anadaiwa kuwa mume wa mtu.
Msanii nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka Odama akiwa kwenye pozi la kimahaba na anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
Wawili hao walinaswa wakiwa kwenye pozi hilo ndani ya Ukumbi wa Ten
Lounge uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam ambapo Odama alikuwa
akimdekea mwanaume huyo kama mtu wake wa karibu.
Wakiwa ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.
Wakiwa ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.
Akimnong'oneza jambo.
Licha ya macho ya watu kuonekana kuwatazama kwa muda mwingi, lakini
wawili hao hawakumjali mtu bali waliendelea kuponda raha huku mikono ya
mwanaume ikiwa haichezi mbali mapajani mwa Odama.
Baada ya kupata picha kadhaa za wawili
hao, Paparazi wetu aliwasogelea na kuwauliza kama wao ni mtu na mwenza
wake, lakini wakabeza na kumtaka awaache wale raha zao.
Msanii nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka.
“Aaaah jamani hebu tuacheni jamani nyinyi kila mkiona watu
wanastarehe, mnaanza kuhisi ni wapenzi, hebu tuacheni jamani,” aliongea
Odama huku akipata mvinyo.Papaa Daudi alipotakiwa kutoa neno, alisema:
“Nakuomba sana, we ndugu mwandishi, ntafute siku nyingine leo hatuna
muda.”