KAMA kawa, leo katika Exclusive Interview tunaye mwigizaji Rose Ndauka ambaye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.Kwenye maisha yake ...
KAMA kawa, leo katika Exclusive Interview tunaye
mwigizaji Rose Ndauka ambaye anatarajia kufunga ndoa hivi
karibuni.Kwenye maisha yake ya sanaa, amepitia mambo mengi ambayo
yanasisimua, katika makala haya utayapata kwa ukamilifu wake:
Mwigizaji maarufu wa filamu za kibongo Rose Ndauka akiwa na mumewe Maliki
ALIVYOANZA KUIGIZA
Ilikuwa ni mwaka 2007, Dairekta na muigizaji wa filamu nchini, Single Mtambalike ‘Rich’ alimshawishi Rose Ndauka aingie kwenye tasnia ya sanaa.
Ilikuwa ni mwaka 2007, Dairekta na muigizaji wa filamu nchini, Single Mtambalike ‘Rich’ alimshawishi Rose Ndauka aingie kwenye tasnia ya sanaa.
Kama bahati, Rose alikuwa akienda kumtembelea rafiki yake katika
Kundi la Kamanda ambalo Rich alikuwa akiigiza, ndipo akashawishiwa
kujiunga na sanaa.
Rich, wasanii wenzake akiwemo Baba Haji, JB, alipomuona kwa mara ya
kwanza aligundua kabisa kuwa Rose anaweza kuigiza ila alikuwa
hajajitambui, hivyo baada ya kuoneshwa njia, fasta akaitumia fursa.
ALIPENDA KUTAZAMA FILAMU
Licha ya kutowahi kuigiza lakini Rose alipenda sana filamu za Kifilipino pamoja na tamthilia mbalimbali za Kizungu zilizokuwa zikiendelea kwenye runinga mbalimbali.
Licha ya kutowahi kuigiza lakini Rose alipenda sana filamu za Kifilipino pamoja na tamthilia mbalimbali za Kizungu zilizokuwa zikiendelea kwenye runinga mbalimbali.
Risasi: Nje ya Rich kukuonesha njia, ujasiri zaidi wa kuendelea na uigizaji uliupata wapi?
Rose Ndauka: Baba Haji ndiyo alisisitiza kuwa naweza, alinipa ushawishi mkubwa, akaniambia nisikate tamaa, kweli nikajitahidi na mpaka leo hii napasua anga za uigizaji hadi kufikia hatua ya kupewa tuzo mbalimbali, namshukuru Mungu.

Risasi: Baada ya kuingia kwenye kundi la akina Rich, ilisemekana kuwa
mlivuka mipaka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na ndiyo maana
ulikuwa na nafasi kubwa ya kucheza filamu, unalizungumziaje hilo?
Rose Nda
Rose Nda
ka: Mh! Siwezi kusema kuwa ni kweli kwa sababu mimi ninachojua Rich alikuwa ni bosi wangu na mpaka leo namuheshimu kama bosi.
Risasi: Wakumbushe wasomaji wa Risasi Jumamosi filamu yako ya kwanza kabisa kuigiza.
Rose: Ilikuwa inaitwa Swahiba, nilicheza kama Aisha msichana aliyekuwa akisoma chuo.
Rose: Ilikuwa inaitwa Swahiba, nilicheza kama Aisha msichana aliyekuwa akisoma chuo.
Risasi: Tukitoka kwenye upande wa filamu na uigizaji, maisha ya
kawaida kwako wewe kama msichana umewahi kuwa na uhusiano na wanaume
tofauti na wengine waliripotiwa katika vyombo vya habari je, ni kwa nini
uliamua kuwabwaga na kuhamia kwa baba mtoto wako (Maliki Bandawe)
unaweza kusema?
Rose Ndauka: Niligundua kuwa hawakuwa na ‘future’ na mimi hivyo
nikaachana nao, nikaamua kutulia na Maliki ambaye ndiye anayetarajia
kunioa soon.
Risasi: Baba mtoto wako mlikutana wapi na una uhakika gani kama ana future na wewe?
Rose Ndauka: Mwanaume mwenye future utamjua tu, kwa huyu naamini nimefika, nilikutana naye Tanga tulikuwa tunafahamiana kabla ya kupendana na kilichotuweka karibu ni kazi hivyo, alivyorusha nanga nikaamua kumkubalia.

Risasi: Wewe ni staa unayependwa na wengi, unazungumziaje usumbufu
kutoka kwa wanaume wakware? Baba mtoto wako anaipokeaje hali hiyo?
Rose: Niliwahi kusumbuliwa na wengi kabla sijaingia kwenye uhusiano
kamili, kuna niliowahi kuwakubalia lakini kuna niliowakataa kwa sababu
hawakuwa na vigezo, baada ya kuwa mama, najiheshimu na baba mtoto wangu
ananiamini anachonikumbisha ni ‘ku-take care’ tu.
Rose: Mh! Siyo kweli, kwanza mimi starehe za klabu nilifanya sana nilipokuwa na umri wa miaka 19-21 baada ya hapo mtu akikwambia aliniona klabu atakuwa anakudanganya, sijakanyaga huko muda mrefu sana.
Risasi: Katika maisha yako umewahi kumfumania umpendaye?
Rose: Nimewahi kumfumania mpenzi (siyo Maliki) mara mbili lakini nilichoshukuru ni kwamba sikuwahi kuachwa katika fumanizi, anayeachwa mara nyingi ni yule ninayemkuta na mpenzi wangu.
Risasi: Je, umewahi kumfumania baba mtoto wako? Ikitokea je utafanyaje?

Rose: Siombi itokee lakini ikishatokea ndiyo nitajua nifanyeje ila
watu wasitegemee kama nikimfumania nitamuacha, nitafanya uchunguzi
nitakapobaini sababu za kufanya hivyo, nitachukua uamuzi sahihi.
Risasi: Umewahi kupata skendo za kutembea na wapenzi wa rafiki zako
akiwemo huyu baba mtoto wako, unalizungumziaje hilo?Rose: Sijawahi na
hata baba mtoto wangu hajawahi kuwa na uhusiano na rafiki yangu yeyote
kabla.