Memba wa Klabu ya Bongo Movie Unity wamepambana vilivyo na kufanikiwa kuchangishana Sh. milioni 7 zilizofanikisha shughuli za msiba wa a...
Memba wa Klabu ya Bongo Movie Unity wamepambana vilivyo na kufanikiwa
kuchangishana Sh. milioni 7 zilizofanikisha shughuli za msiba wa
aliyekuwa mwigizaji, prodyuza na mwandishi wa skripti za sinema za
Kibongo, Adam Philip Kuambiana.
Raisi
wa Bongo Muvi Steve Nyerere akisoma wasifu wa msanii mwenzao aliyekuwa
muigizaji na muongozaji wa Bongo Muvi, Adam Phillip Kuambiana.
Chanzo makini kutoka ndani ya klabu hiyo kilieleza kuwa, mastaa hao
walipangiana kima cha chini kabisa kila mmoja atoe shilingi elfu hamsini
huku wengi wao wakitoa zaidi ya hapo na kufanikiwa kutimiza Sh. milioni
7.
Kuambiana aliyefariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, alizikwa Jumanne wiki hii katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.