Mwezi uliopita Jokate Mwegelo alifunga safari hadi jijini Nairobi, Kenya alikoenda kikazi. Japo hakusema alienda kufanya kazi gani, pich...
Mwezi uliopita Jokate Mwegelo alifunga safari hadi jijini
Nairobi, Kenya alikoenda kikazi. Japo hakusema alienda kufanya kazi
gani, picha za Instagram zinaonesha kuwa alienda kushoot video ya wimbo
wake.
Jokate na Nick Mutuma
Kwenye picha hizo, Jokate anaonekana akiwa na mtangazaji wa TV na muigizaji wa MTV Shuga, Nick Mutuma.
Hivi karibuni Jokate alizungumza na Bongo5 kuhusu alivyojisikia baada
ya kupanda kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta kwa mara ya kwanza jijini
Mwanza na kuelezea mipango ya video. “Nimejisikia furaha sana kwa sababu
nimeweza kuipresent ngoma, I have so many songs ambazo nimerekodi. Pia
wategemee video ya huu wimbo niliouperform. Nimechelewa kuingia kwenye
muziki kwa sababu nilikuwa najaribu kutafuta sound na tone ya muziki
wangu, kwahiyo nilikuwa nafanya majaribio mbalimbali katika studio ili
kujiweka fiti zaidi,” alisema.