post-feature-image
HomeBurudaniHot News

Je, Mwanaume halisi ni yupi? Jamii imetufundisha nini?

Tuko kwenye jamii ambayo tunaambiwa wewe ni mwanaume bila kujua mwanaume ni nani na wajibu wake ni nini. Tumeku...

Upasuaji wa maumbile wapelekea mwanamke kufariki
HAWA HAPA NDIO WANACHAMA WA FREEMASON TANZANIA - LIVE BILA CHENGA
Breakinh News:- Mmiliki wa Shebbyd Blog apata Ajali Mbaya ya Gari aina ya Prado, Wawili wafa Hapo hapo wanne majeruhi.
Tuko kwenye jamii ambayo tunaambiwa wewe ni mwanaume bila kujua mwanaume ni nani na wajibu wake ni nini. Tumekua na kukuzwa huku tukiiga na kujifunza kusiko rasmi kuwa mwanaume halisi.Kila mtu atakuja na maana ya mwanamme halisi kulingana na tamaduni na alivyoambiwa na jamii anayotoka. Je swali langu la msingi, Mwanaume halisi ni yupi?
Nilikaa sehemu na kujifunza kitu ambacho labda kinaweza kukusaidia kama mwanaume mwenzangu. Kuna mambo matano ambayo yanafafanua mwanaume halisi kama ifuatavyo;
Mwanaume halisi ni mtu anayechukua hatua
Hii inamaanisha unapokuwa mwanaume lazima jjue kuwa wewe uchukue hatua za msingi na madhubuti kwa ajili yako, kwa jamii na familia. Usisubiri mtu mwingine achukue hatua fulani wakati wewe upo, ni kitendo cha kujua maamuzi ya msingi na kuyafuata.
Mwanaume halisi huwajibika katika maisha yake
Tuko kipindi ambacho uwajibikaji umekuwa tatizo sana kwetu hivyo kuacha mambo mengi yakiharibika. Jamii imewajibika katika vitu visivyo vya msingi kwa familia zao na kushangaa mambo mbona hayaendi? Kuwajibika kwa ajili ya amani, upendo na familia kwa ujumla. Mwanamme halisi hulisha na kuitimizia familia yake mahitaji ya muhimu kama chakula , makazi, elimu, msimamo wa kiimani na kufundisha maadili yaliyomema kwa familia yake.Mwanamme halisi hutunza watoto aliowazaa na huonyesha upendo kwa watoto hao, haachi watoto wake kila mtaa.
Mwanamme halisi huongoza kwa kujitoa kwa wale anaowaongoza. Uongozi sio kutawala na kufanya kila mtu akuogope na afuate kila unachokiamua, hapana mambo hayako hivyo. Ni uwezo wa kuwadaidia watu wengine namna ambavyo wanatakiwa wawe au waende kwa staili gani kufika kule kunakotakiwa. Kiongozi wa kweli lazima ajitoe kuhakikisha anaowaongoza wanafika wanakohitajika kufika, kwa kutimiza haja zao, kuwapenda na kutokua mbinafsi.
Mwanaume wa kweli anapenda uaminifu. Uaminifu ni kitu ambacho wengi tumepigwa mchanga wa macho na hivyo kudhani ya kuwa uaminfu hauhitajiki kwenye familia zetu au hata kwa wapenzi wetu kwa wale ambao hatujaoa. Kuna mtu mmoja akasema unapokuwa mwaminifu unakuwa na ujasiri wa kusema ninampenda mtu fulani ila usipokuwa mwaminifu hauna ujasiri huo. Je kama wewe ni mwanamme halisi je ni mwaminifu? Najua wengi tumekuwa na stori nyingi na kusema uaminifu hauwezekani ni ndoto tu, lakini kitu kimoja unachotakiwa ujue kama wewe sio mwaminifu kwenye mausiano yako au ndoa yako kuna watu ni waaminifu na ambao familia zao zinaendelea kwa furaha na amani. Wewe ni kuchagua kusuka au kunyoa.
Mwanamme halisi anaacha kumbukumbu nzuri ya kizazi chake. Unachotakiwa kujiuliza je wewe utaacha heshima gani kwa familia yako siku ukiondoka? Au kitu gani kizuri ambacho baba yako alikiacha na ambacho una ujasiri wa kukisema hadharani? Unaweka mpango gani wa kuacha kumbukumbu nzuri juu ya familia yako na wewe mwenyewe?
Hivyo ni baadhi ya vitu nimejifunza sehemu fulani, je jamii zetu tnatambua mwanaume kama nani?
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: Je, Mwanaume halisi ni yupi? Jamii imetufundisha nini?
Je, Mwanaume halisi ni yupi? Jamii imetufundisha nini?
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/07/03.10.13_Mali.Dogon_Country_old_man_and_his_sheep.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/je-mwanaume-halisi-ni-yupi-jamii.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/je-mwanaume-halisi-ni-yupi-jamii.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago