Nyota wa muziki wa Pop kutoka Canada Justin Bieber amepewa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili ikiwa ni...
Nyota
wa muziki wa Pop kutoka Canada Justin Bieber amepewa adhabu ya kuwekwa
chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili ikiwa ni pamoja na kufanya
shughuli za kijamii kwa kosa la kurusha mayai kwenye nyumba ya jirani
yake.
Mahakama ya California pia imemwamuru mwanamuziki huyo kulipa kiasi
cha dola 80,900 kwa uharibifu,kutumikia siku tano za kufanya shughuli za
kijamii na kuhudhuria programu ya kudhibiti hasira.
Bieber mwenye umri wa miaka 20 hakuwepo mahakamani wakati adhabu hiyo inatolewa.
Mwimbaji huo anakabiliwa na kesi mbili za kihalifu mjini Florida na Toronto.