Archive Pages Design$type=blogging

“KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI”.

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali, Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili, Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali, Wakataka na...

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani? 


4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

KUTOKA MITANDAO YA KIJAMII

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: “KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI”.
“KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI”.
https://scontent-b-ams.xx.fbcdn.net/hphotos-xpf1/t1.0-9/1907394_605599452889914_2940562490150391880_n.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/kama-mnataka-mali-mtayapata-shambani.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/kama-mnataka-mali-mtayapata-shambani.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago