Muigizaji maarufu Tanzania, Elizabeth Michae aka Lulu, leo amewekea doa furaha ya kundi la Mapacha baada ya kukana kushirikishwa ...
Muigizaji maarufu Tanzania, Elizabeth Michae aka Lulu, leo amewekea
doa furaha ya kundi la Mapacha baada ya kukana kushirikishwa kwenye
wimbo wao mpya unaoitwa Time For The Money kama kundi hilo linavyodai na
kuandika kwenye poster ya wimbo huo.
“Mwe mwe mwe…!Mbona mnaninyasanyasa…’in Senga’s voice’
I swear sina idea na Huku kushirikishwa….au kuna Elizabeth Michael’Lulu’ mwingine!????
Dah…hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”
Kundi hilo limeeleza kuwa sauti inayosikika ni ya Lulu kama
walivyoambiwa na Tud Thomas aliyefanya wimbo huo. Lakini wamekiri kwamba
hawakuwahi kukutana na Lulu na wala kuwasiliana nae hata siku moja.
Kundi hilo limesema kuwa limeamua kufuta kabisa jina la Lulu kwenye
kazi yao kwa kuwa ameonesha dharau ingawa wao walimuandika kwa heshima.
Linawataka watangazaji wote watakaokuwa wanautambulisha wimbo huo kutolitaja kabisa jina la Lulu wanapoutambulisha wimbo huo.