Staa wa Filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa kutokana na kupenda watoto anaona hawezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu ila...
Staa wa Filamu za Kibongo,
Shamsa Ford amesema kuwa kutokana na kupenda watoto anaona hawezi
kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu ila atakachofanya ni kuzaa tu
mpaka atakapoambiwa hospitali inatosha.
Staa wa Filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
Akichezesha taya na mwandishi wa habari hii, Shamsa alisema kuwa
tangu alipoanza uhusiano na mchumba wake aitwaye Dick kisha kuzaa naye,
walikuwa wamepanga wazae angalau watoto saba ila wapishane kidogo ili
waweze kuwalea vizuri.
“Siwezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu, nitakachofanya nitazaa mpaka basi. Sijali kwamba eti nikizaa nitachuja na kuharibu umbo langu kwani naamini kuwa hata kama nisipozaa bado umri utazidi kwenda na nitakapofikia kuzeeka nitazeeka bila kuwa na watoto,” alisema Shamsa.