Mwanadada mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ MWANADADA mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt ...
Mwanadada mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’
MWANADADA mwenye umbo la utata Bongo, Lulu Semagongo
‘Aunt Lulu’ ameibuka na kueleza kwamba mastaa wamegundua njia mpya ya
kujiuza ambayo ni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Akistorisha na gazeti hili, Aunt Lulu alisema mastaa wengi wa kike
wanajiuza kwenye mitandao ambapo mapedeshee waliopo mikoa mbalimbali
wakishaziona picha zao huwa wanawatafuta kwa udi na uvumba ambapo
wanawapigia simu na kuwatumia fedha na tiketi za ndege ya kwenda na
kurudi.
“Yaani mastaa wa kike hatulali unakuta pedeshee anakutumia tiketi ya
ndege unamfuata mkoani ukienda usiku asubuhi umesharudi Dar unaendelea
na mambo yako ndiyo maana unawaona wasanii wengi wa kike wana fedha
lakini kazi wanazozifanya huzioni,” alisema Aunt Lulu.